Mwanamke wa Kirinyaga auguza majeraha baada ya mumewe kumpasha tohara

September 2024 · 2 minute read

- Monica Mumbi aliripotiwa kushambuliwa na mumewe baada ya wanandoa hao kuwa na ugomvi

- Wawili hao wameoana kwa muda wa miezi 8 na wanaishi kijiji cha Kianugu, mjini Mwea, Kirinyaga

- Alikimbizwa hospitalini ambapo anauguza majeraha

- Polisi wameanzisha msako kwa mshukiwa ambaye alichana mbuga

Polisi katika kaunti ya Kirinyaga wanamsaka mwanamme aliyemvamia mkewe kwa kisu na kukatakata sehemu zake nyeti mnamo Jumatano, Julai 25.

Monica Mumbi, 29, alikimbizwa hospitali ya Kimbimbi baada ya shambulizi la kikatili lililotekelezwa na mwanamme aliyekuwa amemwamini kwa miezi minane kama mume na mlinzi.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

“Ilikuwa usiku aliponishambulia kwa kisu na kunikata,” alisema akiwa hospitalini.

Habari Nyingine: Jamaa amuaibisha mpenziwe kwa chupi zake chafu mtandaoni

Allan Kuyu, afisa wa matibabu alisema Mumbi alipoteza kiasi kikubwa cha damu lakini hali yake ilikuwa imerejea shwari akitaja kwamba alikuwa ameondoka hatarini, Citizen Digital iliripoti mnamo Alhamisi, Julai 26.

“Sehemu zake za siri zilikuwa zikivuja damu na alikuwa tayari amepoteza damu nyingi. Alikuwa na majeraha kote mwilini mwake,” alisema.

Habari Nyingine: Mwanamke Embu ashangaza mahakama kwa kuwasilisha chupi kama ushahidi

Kulingana na Naftali Murimi, jirani wa wanandoa hao, alisikia kelele kutoka nyumbani kwao, ishara kwamba wawili hao walikuwa na mgogoro usiku wa tukio hilo.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibX15f5RmpLCZnpa6rLGMsJhmo5mntq%2FFwKCYZpmlnMK7rYymmKOdopa1onnBmpidmV2urm651KacsJ1doMKuvMCsn5plpKS1or7AZ5%2BtpZw%3D