Mawazo 6 unayofaa kuepuka wakati unapotafuta penzi la kudumu

September 2024 ยท 2 minute read

Kupata penzi la dhati na la kudumu sio jambo rahisi. Hata hivyo, kuna dhana fulani ambazo huenda zinalemaza pakubwa azma yako ya kumpata mpenzi atakayekuheshimu na kukudhamini.

1. Penzi letu halitafaulu

Usikate kauli hata kabla haujamjua vizuri mpenzi wako. Kuingia katika uhusiano na fikira kuwa hutafaulu kama uhusiano wa hapo awali ni sumu inayochangia pakubwa kuharibu uhusiano mchanga. Ni vyema kutumainia kuwa mambo yatachanua.

2. Huyu sio kama mpenzi wangu wa zamani

Usiwahi kufananisha uhusiano wako na mpenzi wako wa sasa na ule wa hapo awali. Kulinganisha uhusiano wako wa sasa na wa awali ni mojawapo ya njia za kuharibu uhusiano wako.

Habari Nyingine: Jinsi wanafunzi wa vyuo vikuu wanafanya uhahaba kidijitali Nairobi

3. Nahitaji mtu ili kukamilika

Ni muhimu kujipenda kwanza kabla ya kumpa mwingine moyo wako. Mambo huenda tenge wakati ambapo mmoja kati ya wapenzi wawili anapohisi kuwa anahitaji mtu ili kukamilika.

4 . Huyu hanifai na wala sio kufu yangu

Taswira unayochora kuhusu mpenzi unayetaka inaweza kuathiri pakubwa furaha yako. Inaweza kukushangaza kuhusu mtu unayeweza kuishia kuwa mpenzi naye.

Waswahili husema; Umdhaniaye siye! Wakati mwingine mtu ambaye hungedhani anaweza kuwa mpenzi wa dhati. Ni bora kumpa mtu nafasi ya kujidhihirisha kabla ya kukata kauli kuwa hakufai.

Habari Nyingine: Vyakula 3 kutoka Mombasa vinavyodaiwa kumfanya mtu 'simba' kitandani

5. Kutarajia makuu kutoka kwa mpenzio

Usitegemee makuu kutoka kwa mpenzi wako. Mahusiano mengi huvunjika kwa sababu ya wapenzi kutarajia kufanyiwa makuu na wapenzi wao.

Habari Nyingine: Wachungaji 2 wazabana mangumi kwa gari waking'ang'ania sadaka

La muhimu na la msingi ni mtu awe anakuheshimu na kukupenda.

6. Utaishia kunidanganya

Iwapo umewahi kudanganywa hapo awali, huenda ukapata dhana kuwa kila mtu hudanganya. Hii inaweza kuzua mtafaruku na mshikemshike na hata kuvunja uhusiano.

Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdibn56fpNmpJqvka%2B8boKMrqWasZ%2BbrqJ5yq6cqa2blnq4rcqaq6JlpaOusbvTmp2urJFivaa62aJkpZldoMKlwcyuZaGsnaE%3D