Jumatano Julai 29: Watu 544 zaidi wapatwa na coronavirus

August 2024 ยท 1 minute read

Watu 544 zaidi wamepatwa na maradhi ya coronavirus kutoka vipimo vilivyofanywa chini ya saa 24 zilizopita.

Watu 12 nao wameweza kufariki kutokana na maradhi hayo.

Habari Nyingine: Jubilee kuaadhibu maseneta waliopinga mswada wa serikali

Waziri wa afya Mutahi Kagwa alsiema huenda kuongezeka kwa wanaopatwa na maambukizi ni kutokana na msimu huu wa baridi.

Aidha Mutahi alionya kuwa idadi ya maambukizi kwa wanawake imeanza kupanda ikilinganishwa na hapo awali.

"Tunaona idadi ya kina dada ambao wanaambukizwa imeanza kuongezeka. Hatujui ni tabia zimeanza kubadilika ua ni nini," alisema Kagwa

Habari Nyingine: Mwanasiasa wa Bungoma aaga dunia

Visa hivyo 544 ni kutoka kwa sampuli 5259 na sasa idadi ya mambukizi Kenya imefikia 19,125.

Waziri aliwataka Wakenya wazingatie masharti yaliyopo kukabili maradhi hayo akisema hilo ndilo litawalinda.

Wakati huo alipuuza kuwepo kwa tiba dhidi ya coronavirus na kupuuza wanaodai kuwa na tiba hizo.

Habari Nyingine: Fejo na rafa: Watoto wawili wasisimua mtandao wakibishana dukani

"Msije mkasema eti sijui dawa inatumika Marekani, ningewaomba mtafute wataalamu wa afya kamilifu katika kujadili suala la ugonjwa huu. Wachaneni na watu wengi wanaibuka na kujiita madakatari," aliongeza waziri huyo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbH16gZhmoa6lkamur7uMo6ylmZlif3p51pqrrmVlaYFuxsCim6Jlp5a9osDWmmSnmV2YvLO7zZqtoqqlqHupwMyl