Molo: Demu arudishwa kwao kwa kutandika mumewe

August 2024 ยท 1 minute read

Mrembo mmoja kutoka eneo la Turi, Molo alilazimishwa kurudi kwa wazazi wake kwa sababu ya mazoea ya kumtandika mumewe kila wakati.

Semasema za mtaani zinaarifu kuwa, mandugu za jamaa waliamua kumfukuza mrembo huyo katili ili wamuokoe ndugu yao.

Habari Nyingine: Nahodha wa Man United, Harry Maguire apatwa na hatia ya kutoa hongo

Kulingana na Taifa Leo, tabia ya mrembo ilianza mwaka jana walipoanza kukorofishana na akamgeuza ngoma kwa kumpiga kila jioni huku akimnyima chakula na mahaba, jambo lililowaudhi mno mashemeji.

Hivi majuzi alimrukia lofa akamtandika hadi akazimia na baada ya ndugu za lofa kumpa huduma ya kwanza walimgeukia mrembo nan kumtaka afunge virago na kurudi kwao.

Habari Nyingine: Rais Uhuru Kenyatta kuhutubia taifa

Inasemekana kidosho hakuwa na wa kumtetea ikabidi aondoke huku mashemeji wakimuonya asijaribu kukanyaga boma la ndugu yao tena.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 073248269.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbIJ6fJJmpKikn2KxprnUZpirrZSewKnDwGaisJmfYri4rYykrK2Znpm2rK2Mpqymnaeae6nAzKU%3D