Kwale: Watoto wa Marehemu Zainab Chidzuga Wapigania Ubunge

August 2024 ยท 2 minute read

Hali si hali katika familia ya aliyekuwa Mwakilishi wa Kike kaunti ya Kwale Zainab Chidzuga huku watoto wake wawili wakigombania kiti cha ubunge cha Matuga.

Haya yalijiri wakati wa sherehe ya kitamaduni ya kuadhimisha siku 40 baada ya kifo cha kiongozi huyo mnamo Jumatatu, Septemba 20, huku wanawe wawili wakitangaza azma yao ya kuwania kiti hicho.

Katika sherehe hiyo, binti yake marehemu ambaye ni mwanahabari wa zamani Mwanaisha Chidzuga aliidhinishwa na familia yake kuwania kiti hicho.

Kwa mujibu wa Taifa Leo ikimnukuu msemaji wa familia hiyo Mwawasa Kishindo, familia hiyo kwa kauli moja ilikubaliana kumuidhinisha Mwanaisha kuvalia kiatu cha uongozi cha mama yake katika kaunti ya Kwale.

Pia soma

Magazeti Jumanne, Septemba 21: Raila Aabiri Rasmi Gari la Kuingia Ikulu

"Baada ya kifo chake tuliketi kama familia tukasema kuwa ikiwa Zainab alikuwa mwanasiasa ni muhimu kwamba mmoja wa watoto wake aendeleze sifa zake katika ulingo huo hiyo ndio maana tulikubaliana awe Mwanaisha," alisema Kishindo kama alivyonukuliwa na Taifa Leo.

Mwanaisha alisema nini kuhusu kuidhinishwa kwake

Akikubali kuidhinishwa kwake, Mwanaisha katika kauli yake alisema atatumia nafasi hiyo kupigania haki za watoto na akina mama.

Hata hivyo, kaka mkubwa wa Mwanaisha, Hassan Chidzuga pia ametangaza kuwa atawania kiti hicho cha ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa 2022.

Hassan alidai kwamba alikuwa karibu sana na mama yake na hivyo anatambua haja ya moyo wake.

Pia aliongezea kuwa kabla ya kifo cha mama yake, walikuwa wanajiandaa kuanza kampeni za 2022.

Zainab Chidzuga ambaye aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 65 alizikwa kulingana na taratibu za dini ya Kiislamu mnamo Ijumaa, Agosti 13 nyumbani kwake Ziwani Golini eneo bunge la Matuga.

Marehemu alifariki dunia Alhamisi, Agosti 12 akipokea matibabu katika hospitali moja mtaani South C.

Pia soma

Magazeti Jumatatu, Septemba 20: Wabunge Washinikiza Kuwe na Ofisi Mbili za Manaibu Rais

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ4N6g5Vmrpqsn6m8bsPAZqSaqpWdsq7BjKaZrqaXmnq7rcinmJtlk522pcbUoJhmr5GltqitzaKYZq2SqruosYykrpqklWO1tbnL